Kamusoko Out Yanga, Aandika Ujumbe Huu Wa Utata.



Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Thabani Scara Kamusoko ameposti ujumbe wa kutatanisha kwenye ukurasa wake Instagram.

Ujumbe huo ambao unawashukuru mashabiki na wana Yanga kwa ujumla unaonyesha waziwazi kuwa tayari kiungo huyo fundi yupo mbioni kuondoka kunako klabu hiyo.

Ujumbe huo unaosomeka. "During my stay here in Yanga  i learnt so many things.i came to #Yanga and learnt how people really appreciate when you really show your commitment to the team jus wana say thanks to all the supporters for the love that you gave me and the love that you still giving me..i really appreciate it a lot..Thank you once again."


Aidha kumekuwa na taarifa zisizo rasimi kua kiubgo huyo amekanusha kuondoka Yanga licha ya kukiri kuandika ujumbe huo wa Shukurani kwa wanayanga.

" Hapana bro mi bado nipo Yanga, toka nimefika hapa nimepewa upendo ambao ni vigumu kuelezea nikaona nami napaswa kusema ahsante na kuonesha kuwa nakubali na kuheshimu thamani nnayopewa sio kama naondoka Yanga, hapana mimi nipo nipo sana. . naomba wataarifu wana Yanga wasielewe tofauti maana wengine wanaweza wakatumia ujumbe wangu kwa mapokeo tofauti na wakatuvuruga"

- Thabaan Kamusoko.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.