Bocco Ataweza Kucheza Dhidi Gendarmerie Nationale Jumatano Hii, Taarifa Kamili Hii Hapa..
Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya Simba John Bocco atakosa mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) dhidi ya Gendarmerie Nationale utakaofanyika Jumatano ya February 21 nchini Djibout.
John Bocco aliumia kifundo cha mguu wa kushoto kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vpl) dhidi ya Mwadui FC uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kushindwa kuendelea na mechi dakika ya 22 na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo na mechi iliisha kwa sare ya mabao mawili kwa mawili ( 2-2).
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma amethibitisha kumkosa nahodha wao kwa mchezo wa marudiano dhidi Gendarmerie National ya Djibout.
“Hutuwezi kulazimisha kumtumia Bocco ni hatari kwake na timu pia tutasubiri mpaka apone kabisa. bado tuna mechi nyingi mbele atatusaidia hatakuwa kwenye kikosi cha timu itakayoondoka kesho kwenda Djibout ”
alisema kocha Masoud.
Mshambuliaji huyo jana Jioni alishindwa kufanya mazoezi na wenzake kwenye uwanja wa Boko Veteran kutokana na maumivu hayo. Ila kwa upande wa Docta amesema Bocco hajaumia sana amewashauri Makocha wasimtumie kwanza wamwache kama wiki moja atakuwa fiti asilimia 100.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.