Ahadi Ya FIFA Kwa Tanzania..
Baada ya Rais wa FIFA Giann Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahmad na viongozi wa nchi nyingine wanachama wa FIFA kutoka sehemu mbalimbali duniani kuwasili Tanzania kwa ajili ya mkutano wa FIFA wa maendeleo ya soka, Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe leo ameongea na waandishi wa habari.
Februar 24 2018 Waziri Mwakyembe alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuwapa taarifa ya kilichojadiliwa ndani ya kikao hicho kuhusiana na maendeleo ya soka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinalikabili shirikisho la soka Tanzania TFF.
Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa FIFA ilikata kutoa pesa kwa TFF muda mrefu lakini baada ya shikisho hilo kujisafisha sasa watakuwa wanapata pesa kama kawaida lakini good news ni kuwa FIFA wameongeza pesa kwa nchini wanachama kama Tanzania sasa itakuwa inapewa dola milioni 1.25 kutoka kupewa dola 250000 kwa mwaka.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.