Jeshi Lamuondoa Raisi Wa Gabon Madarakani.

Leo asubui na mapema, jeshi la Gabon limetangaza kuipindua serikali ya Rais Ali Bongo, ambaye yuko nje ya nchi kwa takribani miezi mbili.
Ali Bongo anapata matibabu nchini Moroko baada ya kuugua kwa gafla alipokuwa ziarani nchini Saudia-Arabia.

Sababu ya mapinduzi hayo, nikutokana na hali ya Rais huyo kudhoofika na baada ya hotuba yake aliyoifanya akiwa Morocco kwa kulitubia taifa lake. Wanajeshi wameeleza kwamba, hali yake hadi muda huu si nzuri na sauti yake katika hotuba hiyo haikuwaridhisha kwa kuonyesha udhaifu wake.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.