Yatakayofanyika 'Simba Day' yawekwa hadharani, Manara ataja sababu za kuichagua Asante Kotoko



Klabu ya soka ya Simba inatarajia kushuka dimbani Agosti 8, mwaka huu kucheza mechi ya kirafiki na klabu bingwa ya Afrika mara mbili, Asante Kotoko ya Ghana katika kusherehekea mahadhimisho ya Siku ya Simba (Simba Day). Akizungumza mbele ya waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, sababu kubwa ya kuichagua timu hiyo kutoka Afrika Magharibi mwaka huu ni ili kunogesha sherehe hizo, kubadili ladha na pia kujipima ubavu kuelekea kwenye michuano ya Kimataifa. Kwa upande wake, Mratibu wa Simba Day, Iman Kajula amesema tayari wiki ya maadhimisho ya Simba Day imeanza leo Agosti Mosi ambapo moja ya kazi watakazozifanya ni kutembelea watoto yatima pamoja na maveterani wa watani wao wa jadi Yanga. Hii ni press conference iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam


No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.