Watano Azam waitwa timu za taifa.
Wachezaji watano wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, watakuwa nje ya timu kwa ajili ya majukumu ya timu zao za Taifa katika mechi za kufuzu Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon.
Nyota hao ni Nahodha Agrey Moris, kiungo mkabaji Mudathir Yahya na mshambuliaji Yahya Zayd, ambao wameshajiunga kambini na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayojiandaa kucheza na Uganda 'The Cranes' Septemba 8 mwaka huu jijini Kampala.
Beki wa kulia Nickolas Wadada, amejiunga na Uganda kujiandaa na mchezo dhidi ya Stars huku kiungo mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu, akitarajia kujiunga na Zimbabwe 'The Warriors', itakayocheza na Congo Brazzaville Septemba 9 mwaka huu.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.