Wasifu wa kocha mpya wa Stars Emmanuel Amunike


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Emmanuel Amunike kuwa kocha mpya wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa mkataba wa miaka miwili. Kocha huyo ambaye anachukua mikoba ya Salum Mayanga ambaye amemaliza mkataba wake na kurudi kwenye klabu yake ya zamani kama mkurugenzi wa ufundi, ametambulishwa leo, Jumatatu mbele ya wanahabari, jijini Dar es Salaam. Akimtangaza Amunike kuwa kocha mpya wa Taifa Stars mbele ya waandishi wa habari, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema wana imani na kocha huyo kuwa ataifikisha mbali timu ya taifa. Akizungumza baada ya kutambulishwa, Amunike ambaye ameichezea timu ya taifa ya Nigeria mechi 27 na kufunga mabao tisa amesema anachohitaji ni ushirikiano wa kuweza kufanikiwa katika kazi yake



No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.