Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.08.2018


Everton wamefikia makubaliano na Barcelona kumsaini mlinzi wa Colombia Yerry Mina, 23, kwa pauni milioni 28.5 kwa mkataba wa miaka mitano. (Sport - in Spanish)

Everton wamewaambia Manchester United kuwa watamchukua beki ya miaka 28 raia wa England Chris Smalling au mlizni wa Sweden Victor Lindelof, 24, ikiwa klabu hizo mbili hazitaafikia makubaliano kuhusu mlinzi raia wa Argentina Marcos Rojo, 28. (Teamtalk)

Manchester United wanajiandaa kutoa ofa kwa beki wa Leicester Harry Maguire, 25, na kwamba sasa wanaweza kulipa pesa nyingi zaidi katika rekodi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Sky Sports)

Wakati huo huo Manchester United wamefanya mawasiliano na Bayern Munich kumsaini mlinzi mwenye miaka 29 mjerumani Jorome Boateng kwa kima cha pauni milioni 44.5. (Bild - in German)


Chelsea wako katika nafasi nzuri kumsaini kwa pauni milioni 75 wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, baada ya Tottenham kujiondoa. (Mirror)


Ofa ya Leicester ya pauni milioni 10 imekataliwa kwa mlinzi wa Brentford Chris Mepham, 20, huku nao Bournemouth wakimmezea mate mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. (Mail)


Wolves wanataka kuilipa Middlesbrough pauni milioni 22 kwa awamu kwa wing'a raia wa Uhispania Adama Traore, 22, badala ya malipo yote kwa jumla kwa kulipa kwanza paunia milioni 18. (Sun)

Crystal Palace wako kwenye mazungumzo kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg raia wa Israel Munas Dabbur, 26. (Mail)


Mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez, 29, anataka kusalia Arsenal na kupigania nafasi yake katika timu licha na klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon kuonyesha dalili ya kumsaini. (Independent)

West Ham wamekamilisha mbio za kumwinda wing'a wa Porto Yacine Brahimi, 28, baada ya kushindwa kukubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria. (Sky Sports)

West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 10 kwa mchezaji wa Le Havre mwenye miaka 20 raia wa Ufaransa Harold Moukoudi. (Mail)


Juventus wanataka pauni milioni 18 kwa kiungo wa kati wa miaka 25 raia wa Italia Stefano Sturaro, ambaye amehusishwa na kuhama kwenda West Ham, Newcastle na Leicester. (Calciomercato)


Real Madrid wameambiwa kulipa pauni milioni 107 ikiwa wanataka kumsaini mshambuliji wa Valencia na Uhispania Rodrigo, 27. (Marca)


Aston Villa na Leeds wote wanataka kumsaini mchezaji wa miaka 25 mlinzi wa Ireland Kaskazini George Saville kutoka Millwall. (Mail)

Aston Villa wanakaribia kumsaini mlinzi wa kikosi cha vijana cha England Axel Tuanzebe, 20 kwa mkopo msimu wote. (Sun)
Bora kutoka Jumapili

Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuwaambia Red Devils kuwa anaweza kufikia makubaliano ya pauni milioni 100 kwa mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 25 kwenda Barcelona. (Daily Star Sunday)


Pia meneja wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kuweka siku ya mwisho kumwinda mlinzi wa England Harry Maguire, 25, ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 80 na Leicester. (Sunday Express)

Manchester United wanakaribia kuafikia makubaliano ya paunia milioni 60 kumsaini mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 29. (Sunday Mirror)


Lakini mbio za Manchester United za pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Barcelona raia wa Colombia Yerry Mina zimefikia kikomo kwa sababu ya mvutano kuhusu malipo ya ajenti. (Sun on Sunday)

Chelsea wanaweka tayari pauni milioni 35 kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27. (Sunday Express)


Chelsea watafanya mazungumzona mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard siku ya Jumamosi na kumpa mchezaji huyo wa miak 27 mkataba kwa pauni 300,000 kwa wiki kumzuia asijiunge na Real Madrid. (Sunday Times - subscription required)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.