Mvua yaharibu tena mechi ya Simba na Ittihad


Kartepe, Uturuki. Mvua kali inayonyesha sasa katika mji wa Kartepe nchini Uturuki, imesababisha mchezo kati ya Simba na Ittihad Riadi de Tanger usichezwe.
Kutokana na hali hiyo, kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amewaambia wachezaji wake wapumzike hadi hali itakapokuwa nzuri.
"Hali imekuwa mbaya mvua inanyesha sana, hivyo mechi haipo mpaka itakapopangwa," alisema meneja wa Simba, Richard.
Huo ulikiwa mchezo wa pili baada ya ule wa awali na Moloudia Oujda FC ambao pia ilivunjima kwa sababu ya mvua katika dakika ya 65 na matokeo yalikuwa sare bao 1-1.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.