Kiba aanza mazoezi rasmi Coastal Union



Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga Ali Saleh Kiba ameanza rasmi kujifua na wenzake kwa ajiri ya maandalizi ya msimu mpya 2018/2019.

Ali Kiba ambaye pia ni Mwanamziki amejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru kwa makubaliano maalum na Coastal Union huku mkataba wake na timu hiyo ukiwa haujawekwa wazi.

Akizungumza na Radio Mlimani, Mwalim Mgunda amesema “Ali Kiba alijiunga na timu siku tatu zilizopita ambapo alijiunga na wenzake na kuanza kufanya mazoezi pamoja.” amesema Mgunda.



Pia amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kumhusu Kiba kwamba atakuwa anacheza michezo ya Dar es Salaam tu, na kusema atacheza michezo yote endapo atakuwa fit.

Kiba,26, atakuwa sehemu ya kikosi cha Coastal msimu ujao ambao wamepanda Ligi kuu msimu huu

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.