Uhamiaji Waviijia Juu Vilabu VPL Kuhusu Vibali Vya Wachezaji Na Makocha Wa Kigeni


Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetakiwa kuzingatia sheria kwa wachezaji na makocha wasio raia wa Tanzania kuhakikisha wanachukuliwa vibali vya kazi na vya kuishi nchini katika muda unaotakiwa. Afisa Habari wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania, Ally Mtanda amesema klabu hizo zinatakiwa kuwa zimeshawaombea vibali hivyo na kuhakikisha watendaji hao kuwa wamepewa vibali hivyo ndipo waanze kazi. Pia Mtanda ametolea ufafanuzi kwa wachezaji ama kocha ambaye msimu uliopita alikuwa klabu nyingine na msimu huu amejiunga timu nyingine, naye anatakiwa kufuata utaratibu huo wa kuomba upya vibali

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.