Yanga Yajitoa Rasmi Kagame Cup 2018, Sababu Hizi Hapa
Klabu ya Yanga Sc, imejitoa kushiriki michuano ya Kagame Cup itakayoanza June 28 hadi July 13. Kikao cha kamati ya Mashindano kilichoketi juzi june 06 kimeazimia kwa pamoja kutoshiriki mashindano hayo na jana wamewasilisha barua kwa TFF kuwajulisha hilo.
-Sababu kubwa inayotajwa na Yanga kutoshiriki michuano hiyo ni ratiba ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) kwani watacheza mchezo wao wa tatu na Gor Mahia jijini Kenya July 18 pia baadhi ya Viongozi wa klabu hiyo wamekelwa na TFF kuwapanga kundi moja na Simba kwa sababu ya kutafuta mapato.
-Akiongea mjumbe wa kamati hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake amesema wamejitoa kushiriki kagame Cup ili kuwapa nafasi wachezaji wao kupumzika kwa ajili ya michezo ya kombe la shirikisho. Pia viongozi wa Yanga wamekelwa na tabia ya TFF ya kuwafanya kama kitenga uchumi kwa kuwapanga na Simba kundi moja wakati wakijua wao wana hali mbaya ya uchumi.
-Wachezaji wa Yanga na bechi la Ufundi tayari wamepewa likizo mpaka June 25 wakati Kagame Cup inatarajia kuanza June 28 Yanga ilipangwa kundi C na watani zao wa jadi klabu ya Simba Sc, St George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.