Mkwasa Awaitwa Wanachama Yanga Kwenye Mkutano Mkuu.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewataka Wanachama wa klabu hiyo wajitokeze kwa wingi kwenye Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumapili, katika ukumbi wa bwalo la Polisi (Police Officers Mess), Osterbay jijini Dar es salaam.
Mkwasa amesema Mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa klabu ya Yanga utaanza saa nne asubuhi.
Amewataka wanachama watakaohudhuria Mkutano huo kuhakikisha wamelipia ada za uanachama kwani hicho ndicho kigezo kitakachotumika kuwaruhusu kuingia.
"Mkutano huu ni muhimu sana kwa mustakabali wa klabu ya Yanga. Nawaomba wanachama wajitokeze kwa wingi kwa sababu kutakuwa na maamuzi mengine ya msingi zaidi ya kuamuliwa na wanachama," amesema.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.