Mtibwa Yaiadhibu Singida United Sasa Kuiwakilisha Nchi Kimataifa.


Klabu ya Mtibwa Sugar imeibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania (ASFC) baada ya kuinyuka klabu ya Singida United kwa jumla ya goli 3-2 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo.


Katika mchezo huo Mtibwa ndio walioanza kupata goli la kwanza kupitia kwa Salum Kihimbwa mnamo dakika ya 22' na Issa Rashid "Baba Ubaya" akaiongezea bao la pili mnamo dakika ya 37'.

Wakati kipindi cha kwanza kikielekea ukingoni Salum Chuku akaipatia bao la kusawazishia Singida United  mnamo dakika 43' mpaka dakika 45 za kwanza zinatamatika Mtibwa wametoka kifua mbele kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili kimeanza kwa timu zote kucheza kwa umakini na dakika ya 70' Tafadzwa Kutinyu akaipatia klabu ya Singida United goli la 2  na kuzifanya timu hizo kuwa sambamba kwa goli 2-2.

Wakati kandanda likielekea kutamatika Mtibwa wakawaduwaza mashabiki wa Singida United kwa kupachika goli wakati wakiwa pungufu baada ya beki wake kupewa kadi nyekundu na Ismail Kihesa kupachika goli lililoipa ubingwa Mtibwa na kuibuka kidedea kwa magoli 3-2.

Na kwa matokeo hayo Mtibwa ndiyo wawakirishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa kwenye michuano ya CAF Confederation Cup.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.