IMEBAINIKA LECHANTRE ANASEPA SIMBA

Image may contain: 1 person, standing
Kocha mkuu wa Klabu ya Simba, Pierre Lechantre leo ataiongoza klabu ya Simba itakapocheza na timu ya Kariobangi Sharks katika michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoanza jana Kenya.

-Pierre Lechatre raia wa Ufaransa alisaini mkataba Simba January 19 ikiwa ni mkataba wa miezi 6 anaolipwa milioni 30 kwa mwezi mkataba huo utaisha mwishoni mwa mwezi June Klabu ya Simba hawajapanga kumuongezea mkataba kocha huyo


-Kocha Pierre Lechatre pia ameomba kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon. Na amefanikiwa kuingia kwenye mchujo wa mwisho wa kumsaka kocha wa timu ya taifa ya Cameroon iwapo atapata itakuwa furaha kwake ila ikikosa Simba wamepanga kuachana naye Rasmi.

-Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abadalah Maarufu kama Try Again amesema mkataba wa kocha huyo na klabu ya Simba utafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu ila hawana mpango wa kumpa mkataba mpya kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.

-Sababu kubwa zinazotajwa klabu ya Simba kutomuongezea mkataba kocha huyo ni kutaka dau kubwa la usajili na kuongezewa mshahara ndani ya klabu hiyo kwa maana hiyo asilimia 90 kocha huyo ataondoka ndani ya klabu ya Simba.

-Baada ya michuano ya Sportpesa Simba watarejea Tanzania kwa mapumziko ya muda mfupi kabla ya kuanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame Cup itafanyika Tanzania ila tarehe ya michuano hiyo bado haijatajwa.

-Tangu Kocha Pierre Lechantre aanze kuifundisha klabu hiyo ameiongoza katika michezo 20 ikiwa 16 ya ligi kuu Tanzania Bara (vpl) na michezo 4 ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) katika michezo hiyo ameshinda mechi 13 ametoa sare mechi 6 na kufungwa mechi 1.

@Yossima Jr

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.