Yanga Yaelekea Mororgoro Baada ya Kipigo Mbeya


Baada ya mchezo dhidi ya Prisons jana, kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo msingine wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unapigwa keshokutwa Jumapili, May 13 kwenye uwanja wa Jamhuri.

Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu iliyoilazimu kucheza michezo mitatu katika kipindi cha siku sita!

Baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kikosi hicho kitarejea jijini Dar es salaam kuungana na wachezaji wengine waliobaki wakiendelea na maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sport.

May 16, saa moja jioni Yanga itakuwa mwenyeji wa Rayon Sport katika uwanja wa Taifa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.