Licha Ya Ubingwa Ila Kuondoka Kukopalepale


Licha ya kutwaa ubingwa akiwa na klabu ya Simba full-back wa timu hiyo Nicholaus Gyan amesemea bado msimamo wake wa kuondoka kunako klabu hiyo bado uko palepale.


Gyan ambaye alitajwa kuondoka hapo awali chini ya uongozi wa kocha Mcameroon, Joseph Omog kutokana na kutokua na maelewano, amekua akipata nafasi ya mara kwa mara chini ya kocha Mfaransa, Pierre Lechantre akitumika kama winga wa kulia.


Raia huyo wa Ghana amesema kuwa anayafurahia maisha ya soka Tanzania huku akifurahia ushindi wa mchezo mmoja baada ya mwingine.

Simba hapo jana imejinyakulia taji la ligi kuu Tanzania bara baada ya ukame wa muda mrefu wa mataji huku ikiwa nyumbani na hii ni baada ya wapinzani wao Yanga ambao walikuwa wakipewa nafasi ya kunyakua kombe hilo kupoteza mchezo muhimu ambao ungeipa presha Simba na hivyo kufanya kushindwa kufikisha idadi ya pointi alizonazo simba hata akishinda mechi zote zilizosalia kwake.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.