Yanga Yachezea Kipigo Kutoka Kwa Waarabu.



Yanga imeanza vibaya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kulazwa mabao 4-0 na USM Algier katika mchezo uliopigwa Jumapili usiku kwenye dimba la Julai 05 nchini Algeria.

USMA iliyotawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza ilijipatia mabao yake kupitia kwa Oussama Darfalou, Farouq Chafal, Abderahmanne Meziane na Zemmammouche aliyefunga bao la nne kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 90.

Matokeo hayo yanaifanya USMA iongoze kundi D ikiwa na alama tatu. Ikifuatia na Gor Mahia yenye alama moja sawa na Rayon Sports.

Yanga inashika nafasi ya nne baada ya mchezo huo mmoja.

Mchezo unaofuata kwa Yanga utapigwa kwenye uwanja wa Taifa May 16 dhidi ya Rayon Sports

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.