Hiki Ndio Kilichobakia Ili Simba Kutangazwa Bingwa VPL 2017/2018


Timu ya Simba imebakisha pointi mbili ili kutawazwa mabingwa wapya wa ligi msimu wa 2017/18 baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Taifa.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha alama 65 ambapo ikipata ushindi katika mchezo ujao dhidi ya Singida United itatawazwa kuwa bingwa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Simba walifika zaidi langoni kwa  Ndanda kikwazo kikawa kwa mlinda mlango Duel Makonga.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi aliifungia Simba bao hilo dakika ya 43 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 baada ya kuwahadaa walinzi wa Ndanda.

Hilo linakuwa bao la 20 msimu huu akiwa ndio kinara wa ufungaji akimzidi sita John Bocco ambaye anamfuatia.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.