YAMETIMIA: ARSENAL WAMTANGAZA MRITHI WA WENGER
Unai Emery amekamilisha kusaini mkataba wa miaka mitatu kukinoa kikosi cha Arsenal. Unai Emery amesaini kandarasi wenye thamani ya Pauni Milioni 15 na kuchukua natasi ya Arsene Wenger aliyeitumikia klabu hiyo kwa miaka takriban 22.
Emery atakua na Kazi kubwa ya kuziba nafasi ya Arsene Wenger aliyejenga heshima kubwa klabuni hapo kwa kipindi kirefu alichokua Arsenal.
Kabla ya kutangazwa Emery hii leo kama mrithi wa Wenger, Mikel Arteta ndiye aliyekua akitajwa zaidi kumrithi Kocha wake wa zamani. Inasemekana Arteta ameshindwana na Uongozi hasa katika suala zima la uendeshwaji wa Klabu hiyo.
“Tunafurahi kumkaribisha Unai Arsenal,” alisema Kroenke. “Amejihakikishia kuwa yeye ni mshindi. Tuna uhakika kwamba, ndiye mtu sahihi kwa hii kazi na kwamba atafanya kazi na kuleta ushindi kwa mashabiki, wafanyakazi na yeyote anayejali kuhusu inachokitaka Arsenal.
“Vitu vingi viliongelewa katika majadiliano na utaratibu mzima; Uelewa wake wa mpira wa miguu, nguvu, juhudi na mapenzi yake ya mpira. Uelewa wake kuhusu klabu na wachezaji wetu, ligi kuu na mchezo katika Ulaya vilikua vya kuvutia sana. Ametuelezea maono yake ya mbele, kutengeneza jukwaa ambalo Wenger alitengeneza na kusaidia klabu kufurahia mafanikio makubwa.”
“Nafurahia kuanza ukurasa mpya katika historia ya Arsenal. Nimekutana na Stan na Josh Kroenke na iko wazi wana lengo kubwa na Arsenal na wana hakika ya kuleta maendeleo ndani ya klabu.”
Emery ndiye aliyekuwa wa kwanza kutangaza kuwa ndiye kocha mpya wa klabu ya Arsenal baada ya kuweka tangazo katika tovuti yake ya unai-emery.com ambayo iliweka maneno yaliyosema “Najisikia fahari kuwa sehemu ya klabu ya Arsenal.”
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.