Alikiba Na Samatta kupimana nguvu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Ukitaja wasanii wa muziki wenye uwezo mkubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu huwezi kuacha kumtaja Alikiba hii ni kutokana na mkali huyo kuonesha kiwango cha juu kila anapocheza kwenye mechi zinazohusisha wasanii wa Bongo Fleva.
Sasa habari nzuri ni kwamba Alikiba utamshuhudia Live kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 9 juni mwaka huu akiwa na Mshambuliaji wa timu ya taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta.
“Tukutane Taifa naomba unichagulie kikosi bora unacho kikubali kutoka team tofauti katika ligi ya TANZANIA bara“amesema Mbwana Samatta.
Wawili hao watakutana kwenye mechi maalumu ya ubalozi wa kujitolea ili kuchangia elimu, hata hivyo orodha ya majina mengine ya wasanii yataendelea kutajwa kadri ya siku zinavyokwenda.
Mbwana Samatta naye amethibitisha taarifa za uwepo wake ambapo amesema “Nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?“.
_______________________________________________________________________________________________
Kwa
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.