Viunzi vitatu vinavyotishia ubingwa Simba
Klabu ya Simba inatakiwa kuvuka viunzi vitatu licha ya kuhitaji pointi tano tu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Simba inasaka pointi tano katika mechi nne zilizobaki itakapocheza na Singida United, Ndanda, Kagera Sugar, Majimaji.
Kwa mantiki hiyo Simba inatakiwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mechi mbili ili kufikisha pointi 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Kiunzi cha kwanza ni hatima ya rufani ambayo Yanga ilikata na kuiwasilisha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kuomba kupewa pointi tatu za mezani katika mchezo dhidi ya Mbeya City waliotoka sare ya bao 1-1.
Yanga ilikata rufani dhidi ya Mbeya City kwa kumuingiza mchezaji ambaye alikuwa amefanyiwa mabadiliko na akaendelea kucheza.
Kanuni ya Ligi Kuu Bara inayoweza kuibeba Yanga kulingana na mazingira ya tukio husika ni ya 14 (25) inayoeleza namna timu inavyoweza kupewa ushindi wa mezani kutokana na makosa ya kumbadilisha mchezaji.
“Timu inaruhusiwa kubadilisha wachezaji watatu (3) tu katika mchezo mmoja, wanaoingia mbadala ni lazima watokane na orodha ya wachezaji 7 (saba) wa akiba.
Timu itakayozidisha kwa kubadilisha zaidi ya wachezaji watatu (3) itapoteza mchezo husika na kutozwa faini,” inafafanua kanuni hiyo.
Endapo Yanga itapata pointi tatu za mezani itafikisha pointi 51, kwa mantiki hiyo Simba italazimika kusaka pointi tisa kwenye mechi nne ilizobakiza hatua ambayo inaweza kubadili upepo.
Pia tatizo la majeruhi linaweza kuitibulia Simba kwa sababu nyota wake wa kikosi cha kwanza wameonyesha kiwango bora, endapo wataumia benchi la ufundi litabadili mfumo wa uchezaji ambao unaweza kuathiri mwenendo mzuri wa timu hiyo katika mbio za ubingwa.
Kiunzi kingine ni mechi nne zilizobaki ambazo zinaweza kuigharimu endapo haitafanya maandalizi ya kutosha au itabweteka na idadi ya pointi ilizonazo mpaka sasa.
Simba inaweza kudondosha pointi kwa kupoteza au kutoka sare jambo ambalo linaweza kuhatarisha uwezekano wa kutwaa ubingwa.
Upinzani utakuwa mkubwa katika mechi mbili dhidi ya Singida United na Majimaji ambazo Simba itakuwa ugenini kwenye viwanja tofauti vya Namfua na Majimaji Songea.
Pia ina mechi mbili ngumu nyumbani dhidi ya Kagera Sugar na Ndanda ambazo katika siku za hivi karibuni zimeonyesha kuimarika kulinganisha na mzunguko wa kwanza.
Kagera Sugar iliyomaliza mzunguko wa kwanza kwa pointi 13, imevuna 15 kwenye mzunguko wa pili, lakini Ndanda inayohaha kujinasua katika janga la kushuka daraja itacheza kufa au kupona ili kupata ushindi.
Hata hivyo, pamoja na changamoto za Simba, Yanga pia itapaswa kufanya kazi kubwa kupata ushindi katika mechi sita ilizobakiza dhidi ya Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Prisons, Mwadui FC, Mbao FC na Azam FC ili kupindua matokeo.
Endapo Yanga itashindwa kupata ushindi kwenye baadhi ya mechi hizo, maana yake itashindwa kupunguza pengo la pointi dhidi ya Simba.
Kocha wa Simba, Pierre Lechantre alisema baada ya kuifunga Yanga, hesabu zake kwenye mbio za ubingwa zimekwenda vizuri na anaamini zitatimia.
Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema timu yake haikatishwi tamaa na matokeo ya mchezo waliofungwa na Simba na itaendelea kupambana hadi dakika ya mwisho kwa kuwa lolote linaweza kutokea.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.