SARE YA YANGA YANOGESHA UTAMU WA MECHI YA AZAM JUMATATU
Pamoja na Yanga kubanwa mbavu ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Maafande wa Ruvu katika uwanja wa Uhuru bado mechi ya Jumatatu dhidi ya Azam FC itakuwa fainali.
Endapo Yanga itashinda mchezo dhidi ya Azam itamaliza nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga baada ya timu zote kufikisha pointi 55.
Mchezo huo ambao utaanza saa 2 usiku unatazamiwa kuwa kama fainali kwani timu zote zina nafasi ya kumaliza namba mbili.
Katika mchezo wa jana mabao ya Yanga yalifungwa na Matheo Anthony na Maka Edward dakika za 19 na 38.
Kwa upande wa Ruvu mabao yao yalifungwa na Khamis Mcha kwa mkwaju wa penati dakika ya 29 na Issa Kanduru dakika ya 48.
Maafande hao wamejihakikishia kusalia kwenye ligi msimu ujao baada ya kufikisha pointi 37 ikiwa nafasi ya nane.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.