Real,Liverpool ni vita ya kisasi cha miaka 37

Na Joseph  michael

-Hiyo ilikuwa ni Mei 27, 1981, bao la Alan Kennedy katika dakika 82, lilitosha kuwapa ubingwa Liverpool katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Parc des Princes.

-Madrid, Hispania. Miaka 37 iliyopita, Real Madrid na Liverpool zilikutana katika fainali ya Kombe la Ulaya.

-Hiyo ilikuwa ni Mei 27, 1981, bao la Alan Kennedy katika dakika 82, lilitosha kuwapa ubingwa Liverpool katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Parc des Princes.

-Ulikuwa usiku mbaya wa mwisho kwa Real Madrid.

-Kipigo hicho kilimaliza ndoto yao ya kutwaa taji la saba na sasa mechi inarudiwa Kiev.

-Real wanataka taji la 13, wakati Liverpool wenyewe wanasaka ubingwa wa sita.

-Tangu wakati huo, Liverpool imeshinda ubingwa mara mbili dhidi ya Roma (1984) na Milan (2005) na wamepoteza mara mbili dhidi ya Juventus (1985) na Milan (2007).

-Real imetwaa taji hilo mara sita; dhidi ya Juventus (1998 na 2017), Valencia (2000), Leverkusen (2002) na Atletico Madrid (2014 na 2016).

-Vikosi vilivyocheza Paris: Real Madrid: Agustin; Garcia Cortes, Sabido, Garcia Navajas, Camacho; Del Bosque, Angel, Stielike, Juanito, Santillana na Cunningham.

-Kocha Mserbia, Vujadin Boskov alimtoa Pineda na kumuingiza Garcia Cortes dakika 87.

-Akiba: Miguel Angel, Isidro, Garcia Hernandez na San Jose hawakucheza.

-Liverpool: Clemence; Neal, Hansen, Thompson, Alan Kennedy; McDermott, Souness, Ray Kennedy, Lee, Dalglish na Johnson.

-Katika dakika 87, Case aliingia kuchukua nafasi ya Dalglish, yakiwa ni mabadiliko pekee yaliyofanywa na kocha Bob Paisley.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.