RAIS MAGUFULI AKUBALI OMBI LA TFF


Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amekubali ombi la TFF kupitia kwa Waziri wa michezo, Harrison Mwakyembe kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Kagera May 19 Uwanja wa Taifa Jijini Dar. Rais Magufuli atawakabidhi kombe mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara (vpl) msimu wa 2017/18 klabu ya Simba.
-Kaimu katibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema pia Rais Magufuli atakabidhiwa kombe la CECAFA la vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys walilotwaa nchini Burundi.
-Mchezo huo unatarajia kuanza saa8 mchana kwa matukio mbalimbali kiingilio cha mchezo huo kimepunguzwa tena na sasa mzunguko ni 2000, 10,000 VIP B na C huku VIP A ikiwa 15000.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.