MSEJA AITAKA NAMBA YA MANULA MAY 19



-Golikipa namba 3 wa klabu ya Simba, Emmanuel Mseja imelitaka bechi la ufundi la klabu hiyo wampe nafasi katika mechi ya may 19 dhidi ya Kagera ili aweze kuonesha kiwango chake. Mseja ameiomba nafasi hiyo kutokana golikipa namba moja Aishi Manula ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi 3 za njano.

-Golikipa Emmanuel Mseja ambaye amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha Simba kutokana na uimara wa Aishi Manula aliyecheza mechi zote 28 za ligi kuu Tanzania Bara (vpl) ameliomba bechi la ufundi wampe nafasi hiyo ili awaoneshe mashabiki wa klabu hiyo yeye sio mtu wa kukaa bechi.




-Mseja alisajiliwa na klabu ya Simba akitokea Mbao Fc ya Mwanza mwanzoni mwa msimu huu amefanikiwa kucheza mechi 4 za mapinduzi Cup tu na ni golikipa namba 3 wa klabu hiyo nyuma ya Aishi Manula na Said Mohamed Nduda ambaye naye hajacheza mechi za kimashindano ndani ya kikosi hicho.

-Pia mchezo huo utaanza saa 8 mchana kwa viingilio vya 3000 mzunguko, 7000 VIP B na C na 15000 VIP A na Klabu ya Simba Sc itakabidhiwa kombe la ligi kuu Tanzania bara (vpl) baada ya kuwa mabingwa wapya wa vpl msimu wa 2017/18.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.