MKUTANO MKUU YANGA WAAHIRISHWA MPAKA JUNI 17 MWAKA HUU


             
Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga ambao awali ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwiki hii sasa utafanyika Juni 17, 2018.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema uamuzi huo umefikiwa kwa pamoja ili kuipa nafasi Yanga kufanya maandalizi ya kutosha katika michuano ya kombe la shirikisho pamoja na kumalizia michezo ya ligi iliyobaki

Mkutano huo awali ulipangwa kufanyika siku ya Jumapili, Mei 06, siku ambayo Yanga itakuwa Algeria ikichuana na UMS Alger.

Mkwasa amesema viongozi watakuwa na majukumu ya utendaji huku wengine wakitarajia kusafiri na timu Jioni ya leo.

Uamuzi huo pia utatoa nafasi kwa Kamati ya uchaguzi kufanya Maandalizi ya kutosha kujua nafasi zipi zipo wazi na zinahitaji kuzibwa.

Kikosi cha Yanga kinaondoka jioni ya leo Alhamisi kuelekea nchini Algeria kupitia Dubai.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.