MKATABA WA YANGA NA MACRON IS DEAD?

Image may contain: 3 people
-Klabu ya Yanga Sc January 16 mwaka huu ilisaini mkataba wa kampuni ya Macron mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo.

-Tangu mwezi January mpaka sasa hamna dalili yoyote ya kampuni hilo kuanza uzalishaji wa vifaa vya Yanga vyenye nembo ya kampuni hiyo mpaka sasa Klabu ya Yanga wanavaa jezi za kampuni ya Joma.


-Katika mkataba huo Yanga walikuwa wanapewa milioni 500 mwaka wa kwanza, milioni 650 mwaka wa pili na milioni 850 kwa mwaka wa tatu ila klabu ya Yanga walikuwa wanapata bonus kila mwaka kulingana na mauzi ya vifaa vya klabu hiyo.

-Kwenye mkataba huo kila mchezaji na bechi la ufundi wangepewa jezi 12 ikiwa jezi 6 (jezi 2 kwa kila aina ya rangi klabu hiyo), jezi 3 za mazoezi na jezi 3 wakati timu inasafiri pia wachezaji na bechi la ufundi wangepewa mabegi na vifaa vingine vinavyotengenezwa na kampuni hiyo..

-Tangu mkataba huo ufungwe January mwaka mpaka sasa hamna dalili yoyote ya kampuni hilo kuidhamini klabu hiyo na habari kutoka kwa mmoja wa maafisa wa kampuni hilo anadai waulizwe Yanga wenyewe ndio wanajua kwa nini kampuni hilo halijawekeza kwenye klabu hiyo.

-Alipoulizwa wajumbe wa kamati Tendaji wa klabu hiyo alidai hawajui kama kunaudhamini kutoka kampuni hilo. hamna fedha yoyote kutoka kampuni hilo na sasa wanahangaika kutafuta fedha sehemu mbalimbali kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiuchumi alidai mjumbe huyo.

-Kwa sasa Klabu ya Yanga inapitia katika wakati mgumu baada ya kuwa na hali mbaya ya kiuchumi ila mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakihoji mamilioni ya Sportpesa na Macron yameenda wapi na viongozi wa klabu hiyo hawajajitokeza kusema kinachoendelea kati ya Yanga na Kampuni hilo la Macron.

-Dili la mkataba huo limekufa ? mkataba unaanza lini umeanza au unaanza msimu ujao? Inatakiwa viongozi wa Yanga waweke wazi kinachoendelea juu yao na kampuni ya Macron maana mashabiki wa klabu hiyo wanajua tayari macron walishaidhamini klabu hiyo.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.