Manula Na Rekodi Zake Simba sc.
Mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula ndiyo kipa pekee ligi kuu aliyedaka mechi zote mpaka sasa ambazo ni 27 na timu yake ikachukua ubingwa.
Kipa huyo aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam FC.
Tangu ajiunge na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi amecheza mechi hizo 27 na kuifanya timu yake kufikisha pointi 65 ambazo hazitaweza kufikiwa na nyingine yeyote.
Amekaa golini kwa jumla ya dakika 2430 na timu yake haijafungwa hata mechi moja.
Makipa wa timu nyingine, wamekuwa wakibadirishana na ambaye amecheza idadi ya mechi nyingi kidogo ni Aron Kalambo wa Tanzania Prisons
Mbali na mechi hizo 27 za ligi kuu, Aishi ameidakia Simba michezo yote ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo ni minne.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.