Mabadiliko VPL Mchezo Kati Ya Simba sc Na Kagera Sugar
Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 29 kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar ambao awali ulipangwa kupigwa Jumapili May 20 2018, umesogezwa nyuma kwa siku moja sasa utapigwa Jumamosi May 19 2018 kwenye uwanja wa Taifa.
Bodi ya ligi pia imebadili muda wa mchezo huo kutoka saa kumi na kuwa saa nane mchana ili kutoa nafasi kwa mabingwa wapya Simba kukabidhiwa kombe.

Tayari TFF imemwandikia barua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Dk Harrison Mwakyembe ikimtaarifu juu ya maombi ya kumualika Rais Jwa amhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo itahusisha pia kukabidhiwa kombe la CECAFA kwa vijana wa Serengeti Boys walilolitwaa nchini Burundi hivi karibuni.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.