Yanga Walalamikia Ratiba Ya Ligi Kuu Kubana.


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga wamelalamikia ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara (vpl) msimu huu kwani inawabana sana. Mjumbe wa kamati tendaji wa klabu hiyo amedai ratiba ya ligi kuu msimu huu sio rafiki kwa klabu yao ila amedai watapambana.

-Mjumbe huyo amedai klabu hiyo inatakiwa kucheza leo na Welayta Dicha nchini Ethiopia kwenye mechi ya mtoano ya Caf Confederation Cup ila wanatakiwa kucheza na Mbeya City siku ya Jumapili April 22 na amedai kikosi kitawasili Tanzania Alhamisi usiku na kuunganisha safari ya kwenda mbeya Ijumaa ya April 20.


-Pia amedai baada ya kucheza na Simba April 29 katika uwanja wa Taifa Dar watasafiri kuwafuata Tz Prisons May 01 mkoani mbeya tena na pia May 05 watacheza na Mbao jijini Dar.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.