Yanga Waitega Simba Kuelekea Mchezo Wao Jumapili..

 

Kuelekea mtanange wa Watani wa jadi, Simba na Yanga utakaopigwa jumapili hii, tayari majigambo na tambo mbalimbali zimeanza kusikika.


Kwa upande wa Yanga wao wameitega Simba kwa kuandika ujumbe wenye fumbo ndani yake, ujumbe huo wenye kusomeka: "Tunatanga rasmi kuwa April 29 ni siku ya.......!" Umetumika kuiwatega Simba ili washindwe kutathimini ni kipi Yanga wanahitaji kwenye mchezo huo.

Je, ni siku ya kucheza na Simba?
Je, ni siku ya kuwafunga Simba?
Je, ni siku ya kutangaza ubingwa?
Au ni siku ya kukabidhi ubingwa?
Yite haya tutayajua baada ya mchezo kumalizika.

Ikumbukwe kuwa mchezo huo utapigwa jumapili aprili 29 kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa taifa na tiketi tayari zimekwisha anza kuuzwa na Selcom.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.