Usajili: Mbao Yampa Kisogo Ndailagije, Yamkabidhid Kijiti Aliyeipandisha Singida United Ligi Kuu.


Kocha wa zamani wa Singida United, Toto Africans na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Fulgence Novatus amechukua mikoba ya kocha Etienne Ndairagije katika timu ya soka ya Mbao FC.

Akizungumza na Jembe FM ya Mwanza Novatus amethibitisha kuwa tayari yeye ni Kicha mkuu wa Mbao na anatarajia kuisaidia timu hiyo Kubaki kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.

Novatus amesema haoni kama lingekuwa jambo la busara kuikataa ofa ya Mbao wakati ambapo ana taaluma inayotosha kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba watu wa Mwanza wanahitaji huduma yake ili timu isishuke daraja.

"Sidhani kama ni jambo la busara kuinyima taaluma yako kuitendea haki, nilichofanya ni kutekeleza matakwa ya taaluma yangu na mahitaji ya watu wa Mwanza, unapokuwa na uwezo wa jambo fulani na lipo kwenye uwezo basi ni lazima ujitoe," Novatus amesema.

Ikumbukwe baada ya mchezo wa ligi kati ya Mbao na Njombe Mji, Mwenyekiti wa klabu hiyo Solly Zephaniah Njashi alisema kuwa uongozi unakusudia kuliboresha benchi la ufundi hivyo inawezekana hiyo ikawa ni sehemu ya kusudio hilo.

Fulgence Novatus baada ya kuisaidia Singida United kupanda ligi daraja la kwanza kutoka la pili, alikwenda kuifundisha timu ya Kimondo FC ya Mbeya lakini haikufanya vizuri na baadae akajiunga na Toto Africans ya Jijini Mwanza.

Alijiunga na Toto Africans ikiwa katika hatari ya kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 14 na alama zao 22 huku wakiwa wamebakiwa na michezo saba na moja ya ahadi zake ilikuwa ni kuiongoza timu hiyo kushinda michezo minne lakini hakufanikiwa na hatimaye ikashuka daraja.

Anakuja Mbao ikiwa katika nafasi ya 14 na alama 23 huku wakiwa wamebakiwa na michezo sita kuhitimisha ligi, swali linabaki je ataweza kuisaidia Mbao kubaki kwenye ligi!?.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.