UCL: Liverpool Yainyuka AS Roma, Salah Ang'ara.


Mshambuliji Mohammed Salah ameiwezesha Liverpool kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya uliofanyika uwanja wa Anfield.

Salah alifunga mabao mawili dakika za 36 na 45 na kusaidia mengine mawili yaliyofungwa na Sadio Mane (61) na Roberto Firmino (67).

Firmino aliifungia Liverpool bao la tano dakika ya 71 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na James Milner.

Kocha wa Liverpool alimtoa Salah dakika ya 78 na kuingiza Danny Ings na kuwafanya Roma kucharuka na kuliandama lango la Majogoo kutokana na kutokuwa na hofu na wachezaji waliobaki.

Roma walipata mabao mawili ya haraka dakika za 81 na 84 yaliyofungwa na Edin Dzeko na Perroti.

Roma itatikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Italia ili kutinga fainali ya michuano hiyo.

Kesho kutakuwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Bayern Munich dhidi ya Real Madrid utakaopigwa  katika uwanja wa Allianz Arena.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.