Stars Baada Ya Kuifunga Congo DR Yapanda Nafasi 9 Viwango Vya Soka Ulimwenguni
Tanzania imepanda kwa nafasi tisa katika viwango vya ubora wa soka Ulimwengu vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kutoka katika nafasi ya 146 hadi nafasi ya 137 kwa kukusanya alama 223 kutoka Alama 186 walizokuwa nazo mwezi uliopita.
Katika kalenda ya FIFA kwa mwezi uliopita Tanzania ilicheza michezo miwili ya kirafiki na kufungwa kwa mabao 4-1 dhidi ya Algeria pamoja na kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo.
Kadhalika kwa upande wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Uganda wameendelea kuongoza wakikamata nafasi ya 74, Kenya imeshika nafasi ya 113, Rwanda wapo nafasi ya 123, Sudan ni 126, Ethiopia nafasi ya 145, Burundi 146 na Sudan Kusini wapo nafasi ya 155.
Afrika
Kwa upande wa Afrika Tunisia wanaongoza wakiwa katika nafasi ya 14 duniani baada ya kupanda kwa nafasi tisa, wanafuatiwa na Senegal Waliopo katika nafasi ya 28, na Congo wapo nafasi 38.
Ulimwenguni bado Ujerumani anaongoza akifuatiwa kwa karibu na Brazil, nafasi ya tatu inashikiliwa na Ubeligiji huku nafasi ya nne wakiwa Ureno na tano Bora inakamilishwa na Argentina
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.