Simba Queens Kushuka Dimbani , Ligi Kuu Ya Wanawake Kuendelea Leo.


Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (Serengeti Premium Lite) Hatua ya Nane Bora inatarajia kuendelea leo Jumamosi Aprili 21,2018 kwa mechi Tatu na mchezo mmoja utachezwa kesho Jumapili Aprili 22,2018.
Leo Kwenye Uwanja wa Karume Evergreen watawakaribisha Alliance ,Wakati kwenye Uwanja wa Mbweni JKT Quenns watakuwa wenyeji wa Simba Queens nayo Kigoma Sisterz ikiwa Uwanja wa Tanganyika kuwaalika Baobab.
Mchezo wa Panama dhidi ya Mlandizi Queens wenyewe utachezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Samora Iringa.
Ligi hiyo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake iliyokuwa na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake dhidi ya Zambia.
Katika hatua nyingine Wadhamini wa Ligi hiyo ya Wanawake kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Bia yake ya Serengeti Premium Lite, imekabidhi mavazi rasmi kwa timu zote.
Meneja Masoko wa Serengeti Anitha Msangi amesema Serengeti inaamini kuwa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake wanachangia kuleta maendeleo ya Mpira wa Wanawake.

Amesema Mashabiki wanayo nafasi kubwa katika maendeleo ya Mpira wa Wanawake na kuwataka waweze kujitokeza kuunga mkono Ligi Kuu ya Wanawake pamoja na kuziunga mkono timu za Wanawake.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.