Okwi Kumbe Sio Mhenga, Avunja Rekodi Za Abdulhaman Mussa Na Simon Msuva Sasa Anyemelea Za Tambwe.


Mshambuliaji hatari zaidi kwa sasa kwenye ligi kuu ya Vodacom, Emanuel Okwi leo amefunga bao lake la 18 katika mchezo ambao Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Taifa.

Okwi sasa amezidi kujiimarisha kileleni katika orodha ya wafungaji bora huku akiwa amedhihirisha ya kuwa yeye sio muhenga bali yupo kazini.

Na hii ni baada ya kuzivunja baadhi ya rekodi za nyota waliopita wa ligi kuu Tanzania bara, ambao miongoni mwa rekodi hizo ni pamoja na zile za washambuliaji Simon Msuva aliyekuwa akikipiga Yanga na Abdulhamani Mussa wa Tanzania Prisson ambao walichukua kiatu cha mfungaji bora kwa kufungana kwa magoli 14 wote katika msimu wa 2016/2017.

Rekodi Anazofukuzia.
Kwa upande mwingine Okwi ameamua kuwaambia kuwa yeye sio mhenga kwa kuzifukuzia rekodi za Murundi Amisi Tambwe ambaye katika misimu miwili aliweka rekodi kwa nyakati tofauti.

Akatika msimu wa 2013/2014 mshambuliaji huyo alitwaa tuzo ya mfungaji bora kwa kutupia kambani jumla ya magoli 19 akiwa mchezaji mwenye magoli mengi hivi karibuni.

Aidha rekodi nyinge anayoifukuzia Okwi ni ile ya mwaka 2015/2016 ambayo Tambwe alivunja rekodi yake mwenyewe ya awali ya goli 19 kwa kufunga goli 21.

Endapo Okwi atazidisha magoli 21 basi atakuwa ndiye mchezaji mwenye kufunga magoli mengi zaidi kwenye ligi kuu Tanzania bara kwa miaka ya hivi karibuni.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.