FT: SIMBA VS MBEYA CITY NA MATOKEO KAMILI HAYA HAPA

FULL TIME

DAKIKA ZA NYONGEZA 2
Dk 90 Okwi anaachia mkwaju, Chaima anaokoa hapa, kona
Dk 89, Kapombe anaambaa pembeni krosi inazuiliwa na kuwa kona
SUB Dk 87, Gyan anakwenda nja na raia mwenzake wa Ghana, James Kotei anaingia kuchukua nafasi yake
Dk 86 Mbeya City inachonga kona safi hapa, lakini goal kick
Dk 85, Manula anaonyesha umahili kwa kupangua mpira mkali wa adhabu na kuwa kona
Dk 82, Simba kama wameamua kurudi nyuma wakisubiri Mbeya City waingie kwenye upande wao


SUB Dk 79 Simba wanamtoa Bocco na nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo
Dk 75, mpira wa kichwa, Bocco anaunganisha lakini anapaisha juuu
KADI Dk 74 Frank Ikobela analambwa kadi njano kwa kucheza kindava dhidi ya Kichuya
SUB Dk 73 Mohamed Hussein anaingia kuchukua nafasi ya Kwasi aliyeumia
Dk 71 Asante Kwasi yuko chini pale, inaonekana kuna tatizo na hii ni mara ya tatu


Dk 68, Gyan anaukuta mpira unazagaa, anaachia mkwaju matata kabisa, gol kick
Dk 67 Okwi anaanchia mkwaju wa adhabu ndogo, unawababatiza mabeki Mbeya City na kuokolewa
Dk 65, Manula analazimika kufanya kazi ya ziada, anaruka juu na kudaka


Dk 64 Okwi anamtoka beki mmoja na kuachia mkwaju mkali lakini nyanya kwa Owen
Dk 62, Kichuya anaingia na kujaribu mkwaju wa mbali, goal kick


SUB Dk 61 Jolam anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Ally Samatta
Dk 53, Okwi anaachia mkwaju mkali kabisa, unagonga mwamba na kurudi uwanjani
Dk 51, Simba wanaonekana kucheza bila ya presha sana lakini wanapoingia upande wa Mbeya City wanakuwa na kasi zaidi
Dk 47, mpira unaonekana kuchezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 45 kipindi cha pili kimeanza na Simba ndiyo wanaanza kushambulia, City wako makini



MAPUMZIKO
Dk ya 45: Inaonyeshwa dakika moja ya nyongeza.
Dk ya 43: Hamidu Mohamed wa Mbeya City anatoka, anaingia Babu Ally.
Dk ya 42: Ally Lundenga wa Mbeya City anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.


Dk ya 41: Simba wanamiliki sehemu kubwa ya mchezo huu.
Dk ya 38: Okwi anawekwa chini, inakuwa faulo kwenda kwa Mbeya City.
John Bocco anaipatia Simba bao la tatu.
Dk ya 35: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Simba wanajipanga kwa kupiga pasi kadhaa.
Mpira wa kona umezaa bao la kwanza kwa Mbeya City.
GOOOOOOOOOOOOOO
Mbeya City wanapata kona.
Kona ya Kapombe ikatua kwa Shiza Kichuya ambaye anampasia Asante Kwasi na kufunga.


GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 30: Bocco anaingia na mpira na kupiga shuti linalotoka nje hatua chache kutoka langoni.
Dk ya 26: Simba wanapata faulo, anapiga Kapombe, mpira unatoka nje inakuwa goal kick.
Dk ya 22: Kasi ya mchezo inaongezeka, Simba wanamiliki mpira muda mwingi.
Dk ya 18: Mbeya City wanapoteza umakini, inapigwa kona langoni kwao.


Simba wanapata bao, mfungaji no Emmanuel Okwi, alimalizia kazi nzuri ya Bocco.
Dk ya 16: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOODk ya 15: Shambulizi kali langoni mwa Mbeya City lakini mpira unaokolewa.
Dk ya 12: Mambo bado hayajanyanga, timu zote zinasomana.
Dk ya 8: Mpira unatoka uakuwa wa kurushwa.
Dk ya 5: Simba wanamiliki mpira na wanjipanga vizuri.
Dk ya 1: Kasi imeanza taratibu.
Mchezo umeanza.
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huu.






Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.