Niyonzima Athibitisha Kupata Ajali.



Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima alipata ajali ya gari juzi maeneo ya Mwenge baada ya gari yake kuacha njia na kuingia kwenye mtaro alipokuwa akirejea nyumbani.

Niyonzima amesema ajali hiyo ilitokea akiwa katika jitihada za kumkwepa mtembea kwa miguu aliyevuka ghafla barabarani.

Kiungo huyo raia wa Rwanda amesema hakupata madhara yoyote katika ajali hiyo.

Amewatoa hofu mashabiki wa Simba waliokuwa wakihoji utimamu wake kwa kusema yuko fiti na anaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa Jumatatu.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.