Mayanga Kutimukia Kenya
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Salum Mayanga anatajwa kuwa moja ya makocha wanaopewa nafasi ya kuinoa AFC Leopards ya Kenya.
Inasemakana Mayanga amemaliza mkataba wake wa kuinoa Stars huku Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) likionekana kutohitaji kuongeza nae mkataba.
Leopards kwasasa inanolewa na Mtanzania Denis Kitambi ambaye ataachana na klabu hiyo mwezi Mei na kuungana na kocha Stewart Hall nchini Bangladesh.
Kitambi na Hall walikutana mara ya kwanza katika klabu ya Azam FC miaka kadhaa iliyopita na sasa wanatarajia kukutana tena katika klabu ya Saif FC ya nchini humo.
Mayanga ni kocha pekee kutoa Afrika aliye katika orodha ya makocha wanaowania kibarua hicho wengine ni Ronalfo Zapata (Argentina),Didier Gomes da Rosa (Ufaransa)
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.