Yanga Kuwafuata Waethiopia Kesho Bila Lwandamina



Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Jumapili kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mchezo huo utapigwa katika mji wa Hawassa Jumatano ijayo April 18. Mji huo uko umbali wa kilometa 275 kutoka mji Mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa.

Yanga inakwenda Ethiopia ikiwa tayari na mtaji wa mabao 2-0 iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa.

Inahitaji ushindi, sare au kufungwa kwa tofauti isiyozidi mabao mawili ili iweze kufuzu.

Kama itapata goli la ugenini itakuwa imejiweka kwenye nafansi nzuri zaidi ya kutinga hatua ya makundi kwani itailazimu Dicha kushinda zaidi ya mabao matatu.

Katika mchezo huo Yanga itakuwa na wachezaji wake wanne, Kelvin Yondani, Said Juma Makapu, Obrey Chirwa na Papi Tshishimbi waliokosa mchezo uliopita wakitumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa nao watarejea katika benchi baada ya kukaa jukwaani mchezo uliopita kutokana na mkanganyiko uliosababishwa na CAF.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.