ABDUL MOHAMED KUBADILISHANA NA PATRICK KAHEMELE?



-Bodi ya klabu ya Azam Fc alimuondoa kwenye nafasi ya meneja mkuu, Abdul Mohamed ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo kutokana sababu za kuingilia majukumu ya kocha na kuruhusu baadhi ya nyota mhimu kuondoka klabuni hapo.

-Baada ya kusimamishwa Abdul Mohamed aliambiwa atapangiwa kazi nyingine. Habari kutoka Bodi ya wakurungezi ya Azam Fc amemuomba aliyewahi kuwa Afisa wa klabu hiyo na katibu wa zamani wa klabu ya Simba, Patrick Kahemele akachukue nafasi ya Abdul Mohamed pale Azam Fc.

-Patrick Kahemele kwa sasa ni mkurungezi wa michezo wa Azam Tv ambapo uongozi wa Azam Tv unatarajia kuandikiwa barua ya kuombwa kwa Patrick Kahemele akawe mtendaji mkuu wa klabu hiyo huku Abdul Mohamed ambaye pia ni mwanahabari akashike nafasi ya Patrick Kahemele Pale Azam Tv.

-Bado haijajulikana kama  Patrik Kahemele atakubali kurudi tena kwenye masula ya Mpira maana wakati anajiuzulu ukatibu wa Simba alisema anapumzika na masula ya mpira afanye shunguli zake nyingine ila akaibukia Azam tv kama mkurungezi wa michezo. Pia bado haijajulikana kama uongozi wa Azam Tv nao utakubali kubadilishana kwa watendaji hao.

-Bodi ya Azam Fc ndio imemuomba Patrick Kahemele kwa bodi ya wakurungezi ya makampuni ya Azam na bodi hiyo imepanga kuja kivingine msimu ujao inatajwa tayari walishamalizana na Kocha Hans Van der Plujm na wanamipango ya kuibadilisha klabu hiyo msimu ujao nje na ndani ya uwanja na kurudisha makali ya Azam Fc ya nyuma.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.