Mfaransa Wa Simba Aipongeza Mbeya City


Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre ameipongeza klabu ya  Mbeya City kufuatia kiwango walichoonyesha kwenye mchezo iliyotoa sare ya goli 1-1 dhidi ya Yanga siku ya Jumapili.

Licha ya kuondolewa kwa m chezaji  mmoja katika nusu ya pili baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu, Mbeya City ilipigana kwa bidii ili kuhakikisha haipotezi mchezo huo na hivyo kuendelea kuiongezea matumaini klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

Akizungumza na mtandao wa Goal, Lechantre ambaye upande wake pia timu yake ilitoa sare na Lipuli Jumamosi, alisema kuwa ni vigumu kuwa pungufu mtu mmoja na kutoka nyuma kisha kusawazisha goli dhidi ya timu kama Yanga.

"Walicheza vizuri sana, walikuwa lengo moja liya ya  kupunguzwa kwa mchezaji mmojo, hata hivyo, walipambana kuhakikisha wanapata pointi," alisema Lechantre.

Simba kwa sasa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 59 huku ikiwa kwenye maandalizi kukabiliana na Yanga ambaye yupo kwenye nafasi ya pili na pointi 48 na michezo miwili mikononi katika mechi yao ya pili ya ligi ya itakayopigwa Aprili 29

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.