MASOUD AFURAHISHWA NA KASI YA UFUNGAJI YA OKWI, BOCCO

Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesifu kasi ya washambuliaji wake John Bocco na Emmanuel Okwi katika kufunga mabao kwenye ligi.

Wawili hao tayari wamefunga mabao 33 kwenye ligi mpaka sasa Okwi akiwa kinara na mabao 19 wakati Bocco akifuatia na mabao 14.

Masoud amesema Okwi ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora lakini kinacho mfurahisha zaidi ni ushirikiano uliopo baina yao kwakua kila mmoja anamtengenezea mwenzake na hakuna uchoyo.

"Nafurahishwa sana ushirikiano baina ya Okwi na Bocco ukiacha kasi ya ufungaji lakini pia wanatengenezeana na hicho ni kitu kikubwa.

"Hata hivyo ushirikiano hauanzii kwa Okwi na Bocco ni timu nzima ndio maana tunapata matokeo ya ushindi mara kwa mara," alisema Masoud.

Baada ya ushindi huo Masoud amesema wanajiandaa na mchezo unaofuata wa ligi dhidi ya Lipuli FC utakaofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa Aprili 21

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.