MANENO YA KOCHA LWANDAMINA KWA YANGA IKIWA NA KIBARUA DHIDI YA WOLAITA DICHA LEO



Aliyekuwa Kocha wa klabu ya Yanga, George Lwandamina, ameandika maneno 13 akiitakia Yanga kheri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha SC utakaopigwa leo mjini Awassa, Ethiopia.

Lwandamina ameandika maneno hayo kupitia Facebook ambayo ni ya faraja kwa Yanga ikiwa ni baada ya takribani wiki sasa tangu aondoke nchini kurejea kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United.

Kocha huyo amesema kuwa ushindi kwa Yanga ni fikra inayofurahisha nafsi ya kila kitu ikiwa ni masaa machache yamesalia kabla ya pambano hilo kuanza.







Yanga itakuwa inashuka dimbani kucheza mchezo wa mkondo wa pili ikitafuta tiketi ya kuingia hatua ya makundi, ambapo katika mechi ya kwanza ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 jijini Dar es Salaam. Mchezo huo utaanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Tanzania.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.