Lwandamina Ailalamikia CAF Kwa Kutoa Taarifa Inayomzuia Yondani Kucheza Dhidi Ya Welayta Dicha.


Kocha wa klabu ya Yanga Sc George Lwandamina amesema beki wake kisiki Kelvin Yondani hana kadi mbili za njano badala yake anayo moja aliyoipata kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers. Hivyo barua ya CAF iliyotumwa klabuni hapo haelewi kwanini wamemuhusisha Yondani kuwa ni moja ya wachezaji ambao wamezuiwa kucheza mchezo ujao dhidi ya Welayta Dicha Sc, anachotambua yeye ni Said Makapu, Papy Tshishimbi na Obrey Chirwa ndiyo wana kadi mbili hivyo kutokana na kanuni za shirikisho hilo hawataruhusiwa kucheza.

Hivyo ameomba uongozi wa Yanga Sc kushughulikia tatizo hilo kabla ya mechi yao ya Jumamosi.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.