KUELEKEA MECHI YA WATANI...SIMBA YAONGOZA KWA UFUNGAJI, NGOME ZIKO SAWA NA MECHI HAITABIRIKI


Wakati watani wa jadi Yanga na Simba zinakutana katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18, Simba ndiyo wanaongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi.

Safu ya ushambulizi ya Simba inaonekana kuwa kali zaidi baada ya wachezaji wake kukwamisha wavuni mabao 58 katika mechi 25.
Watani wao Yanga ambao wamecheza mechi 23 wanafuatia wakiwa na mabao 40 ya kufunga.

Maana yake, watani hao ukijumlisha, wamefunga mabao 98 kwa ujumla na katika mabao ya kufungwa, ngome zao zinaonekana kufanana kwa ubora.

Yanga wamefungwa mabao 13 sawa na Simba. Maana yake, unaweza kusema kiubora wa ulinzi ziko sawa lakini Yanga inaweza kushuka kwa kuwa ina mechi mbili ili kufikisha 25 sawa na Simba.

Kwa upande wa sare, Simba ina 8 na Yanga 9 wakati Simba imeshinda mara 17 huku Yanga wakiwa wameshinda mara 13.

Mechi ya watani hao, mara nyingi inakuwa haitabiriki na imekuwa ikitokea timu inayoonekana bora wakati mwingine kupoteza dhidi ya timu ambayo inaonekana si bora sana.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.