Kabwili kujiunga na wenzake Jumatano
Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Ramadhan Kabwili anatarajiwa kujiunga na kambi ya timu hiyo Jumatano baada ya kuwa nje kutokana na ruhusa maalumu kutoka kwenye benchi la ufundi.
Kabwili ambaye ni kipa namba mbili wa mabingwa wa Tanzania Bara, Dar Young Africans atajiunga na wenzake baada ya kumaliza ruhusa yake ya kuwasaidia mabingwa hao katika mechi zao za kombe la Azam Sports Federations, kombe la Shirikisho Afrika na mechi ya ligi dhidi ya Singida United.
Kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Conrad Ninje ameuthibitishia mtandao huu kurejea kwa Kabwili ambaye anatarajiwa kuwa tegemeo kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya DR Congo kuwania nafasi ya kucheza kombe la Matifa kwa vijana mwakani nchini Niger.
"Kuna urejeo wa Ramadhan Kabwili ambaye Yanga walimuhitaji katika mechi za kimataifa na atajiunga na kambi yetu Jumatano, na mpaka sasa wachezaji wote wapo salama na kambi, tunatarajia atakapojiunga na sisi ataongeza kitu kuelekea katika mchezo wetu na DR Congo baadae mwezi huu," Ninje amesema.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 0-0 Kabwili alionesha kiwango bora kwa kuokoa hatari nyingi ambazo zilielekezwa langoni, hata hivyo katika michezo miwili ya kirafiki kati ya Msumbiji na Morocco kipa Aboutnalib Mshery alionesha kiwango kizuri pia.
Katika hatua nyingine kocha Ninje amesema kambi inaendelea vizuri na wamekuwa na mazoezi mazuri kwani sasa wamekuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku, wakijaribu kutatuta tatizo la ufungaji ambalo limejionesha katika michezo mitatu hadi hivi, huku ukizingatia kuwa wanahitaji kufunga bao katika mchezo wa marudiano.
Mwamuzi kutoka Congo
Aidha toka Shirikisho la soka barani Afrika kutoa orodha ya waamuzi watakaotumika katika mchezo huo, kumeibuka na mjadala wa kwanini Mwamuzi wa Congo Brazzaville Fitial Charel Just Kokolo ameteuliwa kuchezesha pambano hilo, hata hivyo Ninje amesema hawatakuwa na wasiwasi kwani wanaamini haki itatendeka na kumpata mshindi kihalili.
"Sisi tunachohitaji ni fair unajua hatuwezi kupangua na pia lipo nje ya uwezo wetu, ila tunawahitaji wachezeshe kwa haki, atakayeshinda basi apate nafasi ya kusonga mbele, ukiangalia sisi na Congo DR tupo karibu kama ilivyokuwa kwa Congo Brazzaville lakini wao wapo karibu zaidi lakini mimi nawatayarisha vijana wangu tukacheze mpira vizuri tujaribu kutumia nafasi zetu, tusiangalie refarii, sisi wenyewe tujipange kwenda kuwa washindani na kuangalia ni mbinu gani tutazitumia ili tupate ushindi," Ninje ameeleza.
Ikumbukwe kuwa Ngorongoro Heroes watakuwa na kibarua kizito April 22 katika uwanja wa Stade Des Martyrs uliopo katika jimbo la Kinshasa ambapo watalazimika kupata ushindi wa aina yoyote ama sare ya mabao ili kusonga mbele na kukutana na Mali.
Waamuzi wa mchezo huo wa marudiano wote wanatoka Congo Brazzaville ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Fitial Kokolo, waamuzi wasaidizi ni Beaudrel Ntsele Roul na Tritton Franck Audiard Diawa.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.