Je, Mkude Atacheza Mechi Dhidi Ya Njombe Mji? Majibu Haya Hapa..



Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho hapo jana kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Njombe Mji FC leo.

Akizungumza na kipindi cha EFM kupitia E Sports , Manara amesema tayari wameshajiandaa kikamilifu na watajitahidi kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo huo.

Manara ameeleza pia suala la kiungo Jonas Mkude kuanza mchezo huo wa leo kwa kusema kuwa itakuwa ni maamuzi ya Kocha wa timu, japo kwa mujibu wa Daktari hali yake iko vizuri.

"Hali ya Mkude iko vizuri lakini suala la kucheza kesho (leo) ni juu ya maamuzi ya Mwalimu" alisema.

Mkude alianza mazoezi juzi wakati kikosi kikiwa Iringa katika Uwanja wa Samora chini ya Daktari wa timu, Yassin Gembe,


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.