Haji Manara baada ya kusikia Yanga wanapata Tsh milioni 600
Baada ya Tanzania kukosa wawakilishi wa michuano ya Afrika katika hatua ya Makundi msimu uliyomalizika, hatimae leo Club ya Yanga imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa kuitoa Waloitta Dicha ya Ethiopia katika hatua ya mtoano.
Yanga leo wakiwa mjini Awassa Ethiopia katika mchezo wa marudiano wamepoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Esheti Mena dakika ya 2 ila wanafanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla ya agg ya 2-1, hiyo ni baada ya mchezo wa kwanza Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0 uwanja wa Taifa.
Baada ya ushindi huo na kufuzu hatua ya makundi kuna kiasi cha pesa Yanga watapokea kutoka shirikisho la soka barani Afrika CAF ambacho kinatajwa kukadiliwa kufikia milioni 600 za kitanzania, afisa habari wa Simba Haji Manara baada ya kusikia hivyo ameandika ujumbe wa utani kwa Yanga kupitia instagram account yake.
“Hongera watani zetu Gongowazi kwa kufuzu na kujipatia milioni 600..nadhan sasa mtapunguza madeni hususan lile kuu la bilioni tisa toka kwa Yussuf..na ule mkopo wa tiketi za kwenda huko..bila kusahau hata chembe ile mishahara ya kina Lwandamina na player’s..chenji kama itabaki msisahau kina Tegete nao, tukutane VPL 😁😁 @Yangasc@tegete_jerson #yusufmanji
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.